Thursday, September 13, 2018

Maisha ya watu wengi yameathiriwa na watu ambao ni matokeo ya mtu mwenyewe kushindwa kujitambua nakungoja atambulishwe na mtu, HATIMAYE mtu anaanza kufanya mambo mazuri LAKINI ndani yake  hayana USAHIHI mwishowe mtu anaishi Kwa MAJUTO, chunguza na tafakari kuhusu maisha yako utaelewa nachosema......Part 1.
   
Watu hawajali kiwango gani unajua bali  kiwango gani UNAJALI.
Upendo unajali, UNAMFANYA mwingine akuone Wewe ni wa muhimu sana kuliko.
Maneno unayoongea yanatambulisha namna watu watakavyo kuchukulia~ kuku-address Wewe.......Part 2.




   
          HAIMAANISHI HANA KWAO!
 »Kila mtu hapa duniani ana mambo anatamani kuyafanya ili uone uhuru fulani katika maisha anayoishi ! Leo nina ujumbe kwa wale wanaoishi na vijana wa kazi wanafahamika kwa majina mengi kidogo Kama beki tatu, house girl au house boy na majina mengine unayo yajua.
Kitendo cha kuishi na mtu usiyemjua akusaidie kazi KIUKWELI sio jambo la kawaida bali kujitoa MHANGA, sasa inafurahisha kuona uliyemleta anakusaidia na kufanya mambo kuwa mazuri; na ikiwa kinyume na matarajio basi huwa ni maumivu.Hakuna kitu kibaya kama mtu anakusaidia kazi au kukulelea watoto au kusimamia kitu ambacho kutokana na MAJUKUMU mtu amekusaidia na KAFANYA VIZURI HALAFU WAKATI HUO HUO unakosa moyo wa shukurani kumwambia Asante na kukosa kutambua mchango wake; mbaya zaidi akikosea kidogo unamsema weeeeee na kusahau mazuri aliyofanya! Hivi huwazi mara ngapi unaacha nyumbani watoto na mali na wakati mwingine hela ya matumizi kidogo lakini ukirudi mdada wa watu au mkaka wa watu unamkuta kaweka Mambo sawa, cha ajabu unashindwa kumuuliza umeshindaje nayo kazi.
Kibaya zaidi nikumfanyisha mtu kazi toka kumi alfajiri mpaka saa Saba usiku muda wote anafanya kazi na kumgeuza kuwa mashine Wakati wote hata kumpuzika Jamani kumbuka mtu kuja KUFANYA kazi kwako haimanishi hana mahali pa kwenda kumbuka naye anatafuta ili ajikimu, uwe na huruma basi!

           UNAPOISHI NA MTU TAMBUA                                   YAFUATAYO!
#1.Usiishi na mtu kama mtumwa wako, bali kama mwanao au RAFIKI yako.
#2.Hakuna asiyependa kuona anatambuliwa katika MAJUKUMU na nafasi aliyonayo na kupewa anastahiki.
#3.Unachopanda utakuja kuvuna; kama unamfanyia mabaya mtoto wa mwenzio hata wa kwako watu watamfanyia vivyo hivyo.
#4.Jifunze kusema Asante na shukurani kwako~nunua zawadi mpe, msikilize na mpeleke mazingira ya kutambua~refresh mind kama beach au  mbuga Za wanyama-ONYESHA kuwa  naye ni sehemu ya familia.
#5.Usipuuze USHAURI wake maana muda mwingi anakaa na watoto na kitu umeacha amekizoea, chukua jema acha baya.
#6.Akikosea muonye Kwa hekima na ukali pia.
#7.Muelekeze(maneno) na kumuonyesha(kwa Kitendo) anachopaswa.
#8.Anglia ukomavu wa akili na umri wa huyo unakaa naye kwani itakusaidia namna kumsaidia unapobidi.
#9.Muelekeze mipaka yako na yeye kiutendaji~aanzie wapi na aishie wapi.
#10.Washukuru wazazi wake au ndugu ili kuweka uhusiano wa karibu ila EPUKA KUJIINGIZA KWA MAJUKUMU YA KUWATUNZA.
YANGU ni hayo kwa leo.
"Today is short  like it's letters but tomorrow is large like it's letters"